Determination of questions of membership
English
(1)The High Court shall hear and determine any question whether—
(a)a person has been validly elected as a member of Parliament; or
(b)the seat of a member has become vacant.
(2)A question under clause (1) shall be heard and determined within six months of the date of lodging the petition.
(3)Parliament shall enact legislation to give full effect to this Article.
Kiswahili
Uamuzi katika maswali yanayohusiana na uanachama
(1)Mahakama Kuu itasikiliza na kutoa maamuzi katika swali lolote kuhusu—
(a)ikiwa mtu amechaguliwa kama mbunge kwa njia halali; au
(b)ikiwa kiti cha mbunge kimekuwa wazi.
(2)Ombi chini ya ibara ya (1) itasikilizwa na kuamuliwa katika muda wa miezi sita kutoka tarehe ya kuwasilishwa kwa ombi au malalamiko hayo.
(3)Bunge litatunga sheria ili kuwezesha utekelezaji wa Kifungu hiki kikamilifu.