Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi · Kitengo cha Serikali Kinachosimamia Mahakama

Kifungu cha 161

Kif.161

Ofisi na maafisa wa mahakama

Kiswahili

(1)Kitengo cha Mahakama kinajumuisha majaji wa mahakama za ngazi ya juu, mahakimu na maafisa na wafanyakazi wengine katika Kitengo cha Mahakama.

(2)Imebuniwa ofisi ya––

(a)Jaji Mkuu, ambaye atayekuwa Kiongozi wa Kitengo cha Mahakama;

(b)Naibu Jaji Mkuu, atakayekuwa Naibu Mkuu katika Kitengo cha Mahakama;

(c)Msajili Mkuu katika Kitengo cha Mahakama, ambaye atakuwa msimamizi mkuu wa kiutawala na afisa wa uhasibu wa Kitengo cha Mahakama.

(3)Tume ya Huduma za Mahakama inaweza kubuni ofisi zingine za msajili itakavyohitajika.

English

Judicial offices and officers

(1)The Judiciary consists of the judges of the superior courts, magistrates, other judicial officers and staff.

(2)There is established the office of—

(a)Chief Justice, who shall be the Head of the Judiciary;

(b)Deputy Chief Justice, who shall be the Deputy Head of the Judiciary; and

(c)Chief Registrar of the Judiciary, who shall be the chief administrator and accounting officer of the Judiciary.

(3)The Judicial Service Commission may establish other offices of registrar as may be necessary.

Isome ndani ya Sura ya Kumi →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho