Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi na Tatu · Huduma kwa Umma

Kifungu cha 235

Kif.235

Uajiri wa wafanyakazi wa serikali za kaunti

Kiswahili

(1)Kwa kuzingatia taratibu sawa na kanuni zilizoidhinishwa na Sheria ya Bunge, serikali ya kaunti ina wajibu wa––

(a)kubuni na kufutilia mbali nafasi za huduma katika huduma zake za umma;

(b)kuteua watu ili kuhudumu au ili watoe huduma kwa muda mfupi katika ofisi hizo na kuidhinisha uteuzi; na

(c)kudumisha nidhamu pamoja na kuwaondoa watu wanaohudumu katika ofisi hizo au wanaotoa huduma kwa muda mfupi.

(2)Ibara ya (1) haitatumika kwa ofisi au wadhifa wowote ulio chini ya Tume ya Huduma kwa Walimu.

English

Staffing of county governments

(1)A county government is responsible, within a framework of uniform norms and standards prescribed by an Act of Parliament, for —

(a)establishing and abolishing offices in its public service;

(b)appointing persons to hold or act in those offices, and confirming appointments; and

(c)exercising disciplinary control over and removing persons holding or acting in those offices.

(2)Clause (1) shall not apply to any office or position subject to the Teachers Service Commission.

Isome ndani ya Sura ya Kumi na Tatu →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho