Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi na Nne · Usalama wa Kitaifa

Kifungu cha 238

Kif.238

Kanuni za usalama wa kitaifa

Kiswahili

(1)Usalama wa kitaifa ni ulinzi kutokana na vitisho vya ndani na vya nje kwa mipaka ya Kenya na uhuru wa Kenya, watu wake, haki zao, uhuru, mali, amani, uthabiti na maendeleo, na maslahi mengine ya kitaifa.

(2)Usalama wa kitaifa wa Kenya utakuzwa na kuhakikishiwa kulingana na kanuni zifuatazo––

(a)usalama wa kitaifa uko chini ya mamlaka ya Katiba hii na Bunge;

(b)usalama wa kitaifa utatekelezwa kulingana na sheria, na kwa heshima kuu ya utawala wa sheria, demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa kimsingi;

(c)katika kutekeleza majukumu na mamlaka yao, vitengo vya usalama wa kitaifa vitaheshimu tamaduni tofauti za jamii zilizo nchini Kenya; na

(d)uajiri katika vitengo vya usalama vya kitaifa utaonyesha utofauti wa wananchi wa Kenya katika viwango sawa.

English

Principles of national security

(1)National security is the protection against internal and external threats to Kenya’s territorial integrity and sovereignty, its people, their rights, freedoms, property, peace, stability and prosperity, and other national interests.

(2)The national security of Kenya shall be promoted and guaranteed in accordance with the following principles—

(a)national security is subject to the authority of this Constitution and Parliament;

(b)national security shall be pursued in compliance with the law and with the utmost respect for the rule of law, democracy, human rights and fundamental freedoms;

(c)in performing their functions and exercising their powers, national security organs shall respect the diverse culture of the communities within Kenya; and

(d)recruitment by the national security organs shall reflect the diversity of the Kenyan people in equitable proportions.

Isome ndani ya Sura ya Kumi na Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho