Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 25

Kif.25

Haki na uhuru wa Kimsingi ambao hauwezi kudhibitiwa

Kiswahili

Licha ya kifungu kingine chochote katika Katiba hii, haki na uhuru wa kimsingi zifuatazo hazitadhibitiwa––

(a)uhuru kutokana na mateso na unyanyasaji au adhabu zinazokiuka hadhi ya ubinadamu;

(b)uhuru kutokana na utumwa;

(c)haki ya usikilizaji wa kesi kwa usawa; na

(d)haki ya kupewa amri ya kufikishwa mahakamani.

English

Fundamental Rights and freedoms that may not be limited

Despite any other provision in this Constitution, the following rights and fundamental freedoms shall not be limited—

(a)freedom from torture and cruel, inhuman or degrading treatment or punishment;

(b)freedom from slavery or servitude;

(c)the right to a fair trial; and

(d)the right to an order of habeas corpus.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho