Reporting by commissions and independent offices
English
(1)As soon as practicable after the end of each financial year, each commission, and each holder of an independent office, shall submit a report to the President and to Parliament.
(2)At any time, the President, the National Assembly or the Senate may require a commission or holder of an independent office to submit a report on a particular issue.
(3)Every report required from a commission or holder of an independent office under this Article shall be published and publicised.
Kiswahili
Kuripoti kwa tume na ofisi huru
(1)Mwishoni mwa kila mwaka wa kifedha, kila tume na kila anayehudumu katika ofisi huru, atawasilisha ripoti kwa Rais na kwa Bunge, haraka iwezekanavyo.
(2)Kwa wakati wowote, Rais, Bunge la Kitaifa au Seneti inaweza kuitaka tume au anayehudumu katika ofisi huru kuwasilisha ripoti kuhusu suala fulani.
(3)Kila ripoti itakayohitajika kutoka kwa tume au anayehudumu katika ofisi huru chini ya Kifungu hiki, itachapishwa na kutangazwa.