Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 31

Kif.31

Faragha

Kiswahili

Kila mtu ana haki ya faragha, ambayo inajumuisha haki ya—

(a)kutopekuliwa mwilini, na nyumbani au mali yake kutopekuliwa;

(b)kutozuiliwa kwa mali yake;

(c)maelezo yanayohusiana na familia yake, au masuala yake ya kibinafsi kutohitajiwa au kutofichuliwa ila tu iwapo kuna sababu muhimu; au

(d)faragha ya mawasiliano yake kutovunjwa.

English

Privacy

Every person has the right to privacy, which includes the right not to have—

(a)their person, home or property searched;

(b)their possessions seized;

(c)information relating to their family or private affairs unnecessarily required or revealed; or

(d)the privacy of their communications infringed.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho