Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 44

Kif.44

Lugha na Utamaduni

Kiswahili

(1)Kila mtu ana haki ya kutumia lugha na kushiriki katika maisha ya kitamaduni ya chaguo lake.

(2)Mtu anayetoka katika utamaduni au ya lugha fulani, pamoja na wanajamii wenzake, ana haki ya—

(a)kufurahia utamaduni wake na kutumia lugha yake; au

(b)kuunda, kujiunga na kudumisha vyama vya kitamaduni na kilugha, na vitengo vingine vya wanaharakati wa kijamii.

(3)Hakuna mtu atakayemlazimisha mtu mwingine kutekeleza, kuadhimisha au kupitia katika mila zozote za kitamaduni.

English

Language and culture

(1)Every person has the right to use the language, and to participate in the cultural life, of the person’s choice.

(2)A person belonging to a cultural or linguistic community has the right, with other members of that community—

(a)to enjoy the person’s culture and use the person’s language; or

(b)to form, join and maintain cultural and linguistic associations and other organs of civil society.

(3)A person shall not compel another person to perform, observe or undergo any cultural practice or rite.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho