The Constitution of Kenya, 2010

Chapter Four · The Bill of Rights

Article 45

Art.45

Family

English

(1)The family is the natural and fundamental unit of society and the necessary basis of social order, and shall enjoy the recognition and protection of the State.

(2)Every adult has the right to marry a person of the opposite sex, based on the free consent of the parties.

(3)Parties to a marriage are entitled to equal rights at the time of the marriage, during the marriage and at the dissolution of the marriage.

(4)Parliament shall enact legislation that recognises—

(a)marriages concluded under any tradition, or system of religious, personal or family law; and

(b)any system of personal and family law under any tradition, or adhered to by persons professing a particular religion, to the extent that any such marriages or systems of law are consistent with this Constitution.

Kiswahili

Familia

(1)Familia ndio kitengo cha asili na cha kimsingi cha jamii na ndio msingi muhimu katika utaratibu wa kijamii, na itafurahia kutambuliwa na kulindwa na Serikali.

(2)Kila mtu mzima ana haki ya kuoa mtu wa jinsia tofauti na yake na kulingana na idhini isiyolazimishwa ya watu hao wawili..

(3)Wanandoa wana haki sawa wakati wa kuoana, katika ndoa na wakati wa kuvunjwa kwa ndoa hiyo.

(4)Bunge litatunga sheria inayotambua—

(a)ndoa zilizotekelezwa chini ya utamaduni wowote, au mfumo wowote wa kidini, sheria ya kibinafsi au kifamilia; na

(b)mfumo wowote wa sheria ya kibinafsi au kifamilia chini ya utamaduni wowote, au unaofuatwa na waumini wa dini fulani kwa kiwango cha ndoa au mifumo hiyo ya kisheria kuambatana na Katiba hii.

Read it in Chapter Four →

Text: Laws of Kenya: The Constitution of Kenya, 2010. Published by the National Council for Law Reporting (Kenya Law) with the Authority of the Attorney-General.

This is a reading aid, not legal advice. For a legal question, speak to an advocate. Spotted an error? Report a correction