Youth
English
The State shall take measures, including affirmative action programmes, to ensure that the youth—
(a)access relevant education and training;
(b)have opportunities to associate, be represented and participate in political, social, economic and other spheres of life;
(c)access employment; and
(d)are protected from harmful cultural practices and exploitation.
Kiswahili
Vijana
(1)Serikali itachukua hatua, ikijumuisha programu za hatua sawazishi ili kuhakikisha kwamba vijana
(a)wanapata elimu na mafunzo yanayofaa;
(b)wana fursa ya kujumuika, kuwakilishwa na kushiriki katika nyanja za kisiasa, kijamii, kiuchumi na nyanja zingine za maisha;
(c)wanapata ajira; na
(d)wanalindwa kutokana na tamaduni zinazodhuru na kutokana na kunyanyaswa.