Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 108

Kif.108

Viongozi wa vyama

(1)Kutakuwa na kiongozi wa chama cha walio wengi na kiongozi wa chama cha walio wachache.

(2)Kiongozi wa chama cha walio wengi au kiongozi wa walio wengi bungeni kutokana na muungano wa vyama, ndiye atakayekuwa kiongozi wa chama kikubwa zaidi au muungano mkubwa zaidi katika Bunge la Kitaifa

(3)Kiongozi wa walio wachache ndiye atakayekuwa kiongozi wa chama cha pili kwa ukubwa au muungano wa pili kwa ukubwa katika Bunge la Kitaifa.

(4)Utaratibu ufuatao utazingatiwa katika Bunge la Kitaifa––

(a)Spika wa Bunge la Kitaifa;

(b)kiongozi wa chama cha walio wengi; na

(c)kiongozi wa chama cha walio wachache.

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho