Special Bills concerning county governments
English
(1)A special Bill concerning a county government shall proceed in the same manner as an ordinary Bill concerning county government, subject to clauses (2) and (3).
(2)The National Assembly may amend or veto a special Bill that has been passed by the Senate only by a resolution supported by at least two-thirds of the members of the Assembly.
(3)If a resolution in the National Assembly to amend or veto a special Bill fails to pass, the Speaker of the Assembly shall, within seven days, refer the Bill, in the form adopted by the Senate, to the President for assent.
Kiswahili
Miswada maalum inayohusu serikali za kaunti
(1)Mswada maalum unaohusu serikali ya kaunti utashughulikiwa kwa namna sawa na Mswada wa kawaida unaohusu serikali za kaunti, lakini kwa kuzingatia ibara ya (2) na (3).
(2)Bunge la Kitaifa linaweza kurekebisha au kutupilia mbali Mswada maalum uliopitishwa na Seneti kwa uamuzi tu ulioungwa mkono na angalau thuluthi mbili ya wabunge katika Bunge la Kitaifa.
(3)Ikiwa uamuzi wa kurekebisha au kutupilia mbali Mswada maalum utakosa kupitishwa katika Bunge la Kitaifa, Spika wa Bunge ataupeleka Mswada huo, kwa hali iliyopitishwa na Seneti, kwa Rais katika muda wa siku saba ili uidhinishwe.