Miswada ya Fedha
(1)Mswada wa fedha hauwezi kushughulikia suala lingine lolote isipokuwa tu yale ambayo yameorodheshwa katika ufafanuzi wa “Mswada wa fedha” katika ibara ya (3).
(2)ikiwa, kwa maoni ya Spika wa Bunge la Kitaifa, hoja linatoa mwongozo kwa suala lililotajwa katika ufafanuzi wa “Mswada wa fedha”, Bunge linaweza kuendelea tu kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati husika ya Bunge baada ya kuzingatia maoni ya Waziri wa fedha.
(3)Katika Katiba hii, ‘Mswada wa fedha’ unamaanisha, kando na Mswada uliotajwa katika Kifungu cha 218, Mswada ambao unahusu-—
(a)ushuru;
(b)Kutozwa kwa malipo katika hazina ya umma au ubadilishaji au kuondolewa kwa mojawapo ya malipo hayo;
(c)kugawa, kupokea, kutunza, kuwekeza au kutoa pesa za umma;
(d)kutafuta au kudhamini mkopo wowote au ulipaji wake; au
(e)maswala yanayohusiana na maswala yaliyotajwa hapo juu.
(4)katika ibara ya (3), “ushuru”, “fedha za umma”, na “mkopo”, hazijumuishi ushuru wowote, fedha za umma au mkopo uliochukuliwa na kaunti.