Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 116

Kif.116

Sheria kuanza kutumika

(1)Mswada uliopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Rais, utachapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali kama Sheria ya Bunge katika muda wa siku saba baada ya kuidhinishwa.

(2)Kwa kuzingatia ibara ya (3), Sheria ya Bunge inaanza kutekelezwa baada ya siku ya kumi na nne ya kuchapishwa kwake katika Gazeti Rasmi la Serikali, isipokuwa Sheria inapotoa tarehe au wakati tofauti wa kuanza kutekelezwa kwake.

(3)Sheria ya Bunge ambayo moja kwa moja inahusiana na maslahi ya kifedha ya wabunge haitatekelezwa hadi baada ya uchaguzi mkuu ya wanachama wa Bunge utakaofuata.

(4)Ibara ya (3) haitumiki kwa maslahi waliyonayo wanachama wa Bunge wakiwa kama wananchi.

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho