Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 118

Kif.118

Ufikiaji na kushiriki kwa umma

(1)Bunge—

(a)litaendesha shughuli zake kwa njia wazi, na vikao vyake na vya kamati zake vitakuwa wazi kwa umma; na

(b)litawezesha kushiriki na kuhusishwa kwa umma katika shughuli za kutunga sheria na shughuli zingine za Bunge na kamati zake.

(2)Bunge halitazuia umma au vyombo vyovyote vya habari dhidi ya kuhudhuria kikao chochote isipokuwa katika hali za kipekee ambazo Spika anayehusika ataamua kwamba kuna sababu za kuridhisha kuzuia umma au vyombo vya habari.

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho