Lugha rasmi za Bunge
(1)Lugha rasmi za mabunge zitakuwa Kiswahili, Kiingereza na Lugha ya Ishara ya Kenya, na shughuli za maunge zinaweza kuendeshwa kwa Kiingereza, Kiswahili na kwa Lugha ya Ishara ya Kenya.
(2)Iwapo tafsiri tofauti za lugha katika matoleo ya Sheria ya Bunge zitakinzana, toleo la tafsiri lililotiwa saini na Rais ndilo litakalotumika.