Mahakama za Kadhi
(1)Kutakuwa na Kadhi Mkuu na Kadhi wengine wasiopungua watatu kulingana na mwongozo wa Sheria ya Bunge.
(2)Hakuna mtu atakayestahiki kuteuliwa ili kuhudumu katika ofisi ya Kadhi isipokuwa mtu huyo—
(a)ni muumini wa dini ya Kiislamu; na
(b)ana ufahamu wa sheria ya Kiislamu inayotumika katika madhehebu ya Waislamu, ambao kwa maoni ya Tume ya Huduma za Mahakama, unamwezesha mtu huyo kuhudumu katika mahakama ya Kadhi.
(3)Bunge litabuni mahakama za kadhi, na kila mahakama ya Kadhi itakuwa na mamlaka yaliyotolewa kulingana sheria, lakini kwa kuzingatia ibara ya (5).
(4)Kadhi Mkuu na makadhi wengine, au Kadhi Mkuu na Kadhi wengine (wasiopungua watatu) kama inavyoweza kutolewa mwongozo na Sheria ya Bunge, watapewa mamlaka ya kuhudumu katika mahakama ya Kadhi iliyo na mamlaka nchini Kenya.
(5)Mamlaka ya mahakama ya Kadhi yatadhibitiwa ili kushughulikia maswala kuhusu sheria ya Uislamu yanayohusiana na hadhi ya kibinafsi, ndoa, talaka au urithi katika kesi ambazo pande zote husika zinakiri dini ya Kiislamu na zinatii mamlaka ya mahakama za Kadhi.