Kuundwa kwa Tume ya Huduma za Mahakama
(1)Tume ya Huduma za Mahakama imebuniwa.
(2)Tume hiyo itajumuisha—
(a)Jaji Mkuu, atakayekuwa mwenyekiti wa Tume;
(b)Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu Zaidi aliyeteuliwa na majaji wa Mahakama ya Juu Zaidi;
(c)Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa aliyeteuliwa na majaji wa Mahakama ya Rufaa;
(d)Jaji mmoja wa Mahakama Kuu na hakimu mmoja, mwanamke mmoja na mwanaume mmoja, walioteuliwa na wanachama wa muungano wa majaji na mahakimu;
(e)Mwanasheria Mkuu;
(f)mawakili wawili, mwanamke mmoja na mwanaume mmoja, kila mmoja akiwa na uzoefu wa angalau miaka kumi na mitano, walioteuliwa na chama kinachowajibika kisheria kudhibiti taaluma ya mawakili;
(g)mtu mmoja aliyeteuliwa na Tume ya Huduma za Umma; na
(h)mwanamke mmoja na mwanaume mmoja watakaowakilisha umma, na wasiokuwa wanasheria, watakaoteuliwa na Rais kwa idhini ya Bunge la Kitaifa.
(3)Msajili Mkuu wa Kitengo cha Mahakama ndiye atakayekuwa Katibu wa Tume hiyo.
(4)Wanachama wa Tume hiyo, isipokuwa Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu, watahudumu kwenye ofisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano na watastahiki kuteuliwa ili kuhudumu kwa muhula mwingine mmoja wa miaka mitano, mradi tu wawe wamehitimu,