Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi na Tatu · Huduma kwa Umma

Kifungu cha 237

Kif.237

Tume ya Huduma kwa Walimu

Kiswahili

(1)Tume ya Huduma kwa Walimu limebuniwa.

(2)Majukumu ya Tume hiyo ni—

(a)kuwasajili walimu waliopata mafunzo;

(b)kuajiri walimu waliosajiliwa;

(c)kuwatuma walimu walioajiriwa na Tume hiyo ili wahudumu katika shule au taasisi yoyote ya umma;

(d)kuwapandisha vyeo na kuwahamisha walimu;

(e)kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya walimu; na

(f)kuwafuta kazi walimu.

(3)Tume hiyo––

(a)itakagua viwango vya elimu na mafunzo ya watu wanaojiunga na huduma ya ualimu;

(b)itakagua hitaji la walimu na idadi ya walimu waliopo; na

(c)itashauri serikali ya kitaifa kuhusu masuala yanayohusiana na taaluma ya ualimu.

English

Teachers Service Commission

(1)There is established the Teachers Service Commission.

(2)The functions of the Commission are—

(a)to register trained teachers;

(b)to recruit and employ registered teachers;

(c)to assign teachers employed by the Commission for service in any public school or institution;

(d)to promote and transfer teachers;

(e)to exercise disciplinary control over teachers; and

(f)to terminate the employment of teachers.

(3)The Commission shall—

(a)review the standards of education and training of persons entering the teaching service;

(b)review the demand for and the supply of teachers; and

(c)advise the national government on matters relating to the teaching profession.

Isome ndani ya Sura ya Kumi na Tatu →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho