Kuundwa kwa Baraza la Usalama wa Kitaifa
(1)Baraza la Usalama wa Kitaifa limebuniwa.
(2)Baraza hilo linajumuisha—
(a)Rais;
(b)Naibu wa Rais;
(c)Waziri anayewajibika kuhusu ulinzi;
(d)Waziri anayewajibika kuhusu masuala ya kigeni;
(e)Waziri anayewajibika kuhusu usalama wa ndani;
(f)Mwanasheria Mkuu;
(g)Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Kenya;
(h)Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Upelelezi za Kitaifa; na
(i)Inspekta-Jenerali wa Huduma za Polisi za Kitaifa.
(3)Baraza hilo litakuwa na mamlaka ya kusimamia vitengo vya usalama wa kitaifa na kutekeleza majukumu mengine yoyote yatakayotolewa na sheria ya kitaifa.
(4)Rais ataongoza mikutano ya Baraza.
(5)Baraza litateua katibu wake.
(6)Baraza hilo—
(a)litaunganisha sera za humu nchini, za kigeni na za kijeshi zinazohusiana na usalama wa kitaifa ili kuviwezesha vitengo vya usalama wa kitaifa kushirikiana na kufanya kazi kikamilifu; na
(b)litatathmini na kukadiria malengo, kujitolea katika utendakazi, na hatari kwa Jamhuri kwa kuzingatia uwezo halisi na uwezo unaokuzwa, wa usalama wa kitaifa.
(7)Baraza hilo litatoa ripoti kwa Bunge kila mwaka kuhusu hali ya usalama nchini Kenya.
(8)Kwa idhini ya Bunge, Baraza linaweza—
(a)kuvipeleka vikosi vya kitaifa nje ya Kenya kwa madhumuni ya—
(i)kutoa msaada wa kudumisha amani katika eneo hili au kimataifa; au
(ii)shughuli zingine za kutoa msaada; na
(b)kuidhinisha kuletwa kwa vikosi vya kigeni nchini Kenya.