Malengo, mamlaka na ufadhili wa tume na ofisi huru
(1)Malengo ya tume hizo na ofisi huru ni—
(a)kulinda mamlaka makuu ya wananchi;
(b)kuhakikisha kwamba vitengo vyote vya serikali vinazingatia kanuni na maadili ya kidemokrasia; na
(c)kukuza mfumo wa kikatiba.
(2)Tume hizo na wanaohudumu katika ofisi hizo huru—
(a)wako chini ya Katiba hii na sheria tu; na
(b)wako huru na hawako chini ya maelekezo au udhibiti wa mtu au mamlaka yoyote.
(3)Bunge litatenga fedha za kutosha ili kuwezesha kila tume na ofisi huru kutekeleza majukumu yake na bajeti ya kila tume na ofisi huru itakuwa kando.