Haki ya kuishi
(1)Kila mtu ana haki ya kuishi.
(2)Maisha ya mtu huanza wakati mimba inapotungwa.
(3)Mtu hatauawa kimakusudi, isipokuwa kwa njia inayoidhinishwa na Katiba hii au kwa sheria nyingine iliyoandikwa;
(4)Uavyaji mimba hauruhusiwi, isipokuwa kwa maoni ya mtaalamu wa masuala ya afya kuwa kuna haja ya matibabu ya dharura, au maisha au afya ya mama imo hatarini, au ukiwa umeidhinishwa na sheria nyingine iliyoandikwa;