Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 34

Kif.34

Uhuru wa vyombo vya habari

(1)Uhuru wa vyombo vya habari, ikijumuisha vyombo vya kuchapisha, vya kielektroniki na vinginevyo unahakikishwa, lakini haijumuishi njia yoyote ya kujieleza iliyotajwa katika Kifungu cha 33 (2).

(2)Serikali—

(a)haitadhibiti au kuzuia mtu yeyote anayehusika katika utangazaji, uchapishaji au usambazaji wa chapisho lolote au usambazaji wa habari kwa kutumia njia yoyote; au

(b)haitamwadhibu mtu yeyote kwa kutoa maoni au mtazamo wake, au kwa sababu ya masuala yaliyomo kwenye matangazo, chapisho au usambazaji.

(3)Utangazaji na vyombo vingine vya habari vya kielektroniki vina uhuru wa kuanzishwa chini ya taratibu za upataji leseni ambazo—

(a)ni muhimu ili kudhibiti masafa ya utangazaji wa moja kwa moja na aina zingine za usambazaji wa masafa; na

(b)hazidhibitiwi na serikali, au kwa madhumuni ya kisiasa au ya kibiashara.

(4)Vyombo vyote vya habari vinavyomilikiwa na Serikali—

(a)vitakuwa huru kuamua kuhusu yaliyomo kwenye habari na matangazo yao au mawasiliano mengine;

(b)havitaegemea upande wowote; na

(c)vitatoa nafasi sawa ya kuwasilisha mitazamo tofauti na maoni yanayopinga maswala fulani.

(5)Bunge litatunga sheria itakayosimamia kuundwa kwa shirika ambalo—

(a)halitadhibitiwa na serikali, madhumuni ya kisiasa au ya kibiashara;

(b)litaangazia maslahi ya sehemu zote za jamii; na

(c)litaweka viwango vya vyombo vya habari na kudhibiti na kufuatilia ufuataji wa viwango hivyo.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho