Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 35

Kif.35

Uhuru kupata habari

(1)Kila mwananchi ana haki ya kupata—

(a)habari au maelezo yaliyo na Serikali ; na

(b)habari au maelezo ambayo mtu mwingine anayo na ambayo yanahitajika ili kutekeleza au kulinda haki yoyote au uhuru wowote wa kimsingi.

(2)Kila mtu ana haki ya kudai marekebisho au kufutuliwa mbali kwa habari zozote za uongo au zinazopotosha na ambazo zinamwathiri mtu huyo.

(3)Serikali itachapisha na kutangaza taarifa yoyote muhimu inayoathiri taifa.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho