Hatua za haki za kiutawala
(1)Kila mtu ana haki ya hatua za kiutawala ambazo ni za haraka, zenye ufanisi, za kisheria, zifaazo na zenye utaratibu ulio na usawa.
(2)Ikiwa haki au uhuru wa kimsingi wa mtu umeathiriwa au unaweza kuathiriwa na hatua ya kiutawala, mtu huyo ana haki ya kupewa sababu za hatua hiyo
(3)Bunge litatunga sheria ili kuwezesha utekelezaji wa haki katika ibara ya (1) na sheria hiyo—
(a)itatoa nafasi ya kukaguliwa kwa hatua hiyo ya kiutawala na mahakama au, ikiwezekana, mahakama maalum ya kiwango cha chini ambayo ni huru na isiyoegemea upande wowote; na
(b)itakuza utawala wenye ufanisi.