Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 100

Kif.100

Kukuza uwakilishi wa jamii zilizotengwa

Bunge litatunga sheria ili kukuza uwakilishaji Bungeni wa—

(a)wanawake;

(b)watu wenye ulemavu;

(c)vijana;

(d)vikundi vya watu wa kikabila na vya walio wachache; na

(e)jamii zilizotengwa.

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho