Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 102

Kif.102

Muhula wa Bunge

(1)Muhula wa kila Bunge la Kitaifa na Seneti unamalizika katika tarehe ya uchaguzi mkuu unaofuata..

(2)Kenya ikiwa vitani, kwa uamuzi unaoungwa mkono na angalau wabunge wasiopungua thuluthi mbili ya wabunge wote katika kila kitengo cha bunge, Bunge linaweza kuongeza kipindi cha Bunge kwa muda usiozidi miezi sita kwa wakati huo.

(3)Muhula wa bunge hautaongezwa kwa jumla ya zaidi ya miezi kumi na miwili chini ya ibara ya (2).

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho