Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 103

Kif.103

Mbunge kuondoka ofisini

(1)Kiti cha Mbunge kitakuwa wazi—

(a)ikiwa mwakilishi wadi huyo atafariki dunia;

(b)ikiwa, katika kipindi chochote cha vikao vya Bunge, mwanachama huyo hajahudhuria vikao vinane vya kitengo cha bunge husika bila ruhusa ya Spika wa kitengo chake cha bunge kwa njia ya maandishi, na ameshindwa kutoa sababu ya kuridhisha kwa kamati husika kuhusu kutohudhuria kwake;

(c)ikiwa mwanachama huyo ameondolewa ofisini vinginevyo chini ya Katiba hii au chini ya sheria iliyotungwa chini ya Kifungu cha 80;

(d)ikiwa mbunge huyo atajiuzulu kwa kumwandikia barua Spika;

(e)ikiwa, baada ya kuchaguliwa katika Bunge––

(i)kama mwanachama katika chama cha kisiasa, mwanachama huyo ajiuzulu kutoka kwa chama hicho au achukuliwe kuwa amejiuzulu kutoka kwa chama hicho kama inavyobainishwa kulingana na sheria inayozingatiwa katika ibara ya (2); au

(ii)kama mgombea huru, mwanachama huyo atajiunga na chama cha kisiasa;

(f)baada ya kukamilika kwa muhula wa Bunge husika; au

(g)ikiwa mbunge huyo hatastahiki tena kuchaguliwa katika uchaguzi wa Bunge chini ya Kifungu cha 99 (2) (d) hadi (h).

(2)Bunge litatunga sheria litakalotoa hali ambazo mwanachama wa chama cha kisiasa atachukuliwa kuwa amejiuzulu kutoka chama hicho, kwa madhumuni ya ibara ya (1) (e).

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho