Haki ya kumwondoa mbunge mamlakani
(1)Wapiga kura chini ya Vifungu vya 97 na 98, wana haki ya kumwondoa mamlakani mbunge anayewakilisha eneobunge lao kabla ya kukamilika kwa muhula wa kitengo husika cha Bunge.
(2)Bunge litatunga sheria itakayotoa sababu ambazo zinaweza kupelekea kuondolewa kwa mwanachama wa bunge na taratibu itakayofuatwa.