Maspika na Manaibu Spika wa Bunge
(1)Kutakuwepo—
(a)Spika wa kila kitengo cha Bunge, atakayechaguliwa na Kitengo hicho kulingana na Kanuni za Vikao vya Bunge, kutoka miongoni mwa watu wanaostahiki kuchaguliwa kama wanachama wa Bunge lakini ambao sio wabunge; na
(b)Naibu Spika katika kila Kitengo cha Bunge, atakayechaguliwa na Kitengo hicho kutoka miongoni mwa wabunge katika Kiengo hicho kulingana na Kanuni za Vikao vya Bunge.
(2)Kiti cha Spika au Naibu wa Spika kitakuwa wazi—
(a)wakati Kitengo cha Bunge kipya kitakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi;
(b)ikiwa anayehudumu, kama mwanachama wa Kitengo husika, ataondoka ofisini chini ya Kifungu cha 103;
(c)ikiwa Kitengo husika kitaamua, kwa uamuzi ulioungwa mkono na kura za angalau wabunge wasiopungua thuluthi mbili; au
(d)ikiwa anayehudumu atajiuzulu kwa kukiandikia barua Kitengo husika.