Kuongoza Vikao Bungeni
(1)Katika kikao chochote cha Kitengo cha Bunge—
(a)Spika ndiye anayeongoza;
(b)ikiwa Spika hayupo, Naibu wa Spika ataongoza; na
(c)Spika na Naibu Spika wasipokuwepo, mwanachama mwingine wa Kitengo hicho aliyechaguliwa na Kitengo hicho ataongoza;
(2)Katika kikao cha pamoja kati ya Vitengo vya Bunge, Spika wa Bunge la Kitaifa ataongoza, akisaidiwa na Spika wa Bunge la Seneti.