Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 109

Kif.109

Matumizi ya mamlaka ya kutunga sheria

(1)Bunge litatekeleza mamlaka yake ya kutunga sheria kupitia kwa Miswada itakayopitishwa Bungeni na kuidhinishwa na Rais.

(2)Mswada wowote unaweza kutoka kwa Bunge la Kitaifa.

(3)Mswada usiohusu serikali za kaunti utazingatiwa tu katika Bunge la Kitaifa, na kupitishwa kulingana na Kifungu cha 122 na Kanuni za Vikao vya Bunge.

(4)Mswada unaohusu serikali za kaunti unaweza kutoka kwa Bunge la Kitaifa au Seneti, na utapitishwa kulingana na Vifungu vya 109 hadi 113, Vifungu vya 122 hadi 123 na Kanuni za Vikao vya Bunge.

(5)Mswada unaweza kuwasilishwa na mwanachama yeyote au kamati yoyote ya Kitengo husika cha Bunge, lakini Mswada unaohusu fedha unaweza kuwasilishwa tu katika Bunge la Kitaifa kwa mujibu wa Kifungu cha 114.

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho