Miswada ya kawaida inayohusu serikali za kaunti
(1)Ikiwa Kitengo kimoja kitapitisha Mswada wa kawaida kuhusu kaunti, na Kitengo cha pili––
(a)kiukatae Mswada huo, basi utapelekwa katika kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 113; au
(b)kiupitishe Mswada huo baada ya kuurekebisha, utarejeshwa kwa Kitengo kilichoutoa Mswada huo mwanzoni, ili kutathminiwa tena.
(2)Ikiwa, baada ya Kitengo kilichotoa Mswada huo kuutathmini tena chini ya ibara ya (1) (b), Kitengo hicho––
(a)kitaupitisha Mswada kama ulivyorekebishwa, Spika wa Kitengo hicho ataupeleka kwa Rais katika muda wa siku saba ili uidhinishwe; au
(b)kitaukataa Mswada huo kama ulivyorekebishwa, Mswada huo utatumwa kwa kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 113.