Kamati za upatanishi
(1)Ikiwa Mswada utatumwa kwa kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 112, Maspika wa Vitengo vyote viwili watateua kamati ya upatanishi itakayohusisha idadi sawa ya wanachama wa Vitengo vyote viwili ili kujaribu kutengeneza toleo jingine la Mswada litakalopitishwa na Vitengo vyote viwili.
(2)Ikiwa kamati ya upatanishi itakubali toleo la Mswada huo, kila Kitengo kitapiga kura ili kupitisha au kukataa toleo hilo la Mswada.
(3)Ikiwa Vitengo vyote viwili vitaidhinisha toleo hilo la Mswada lililopendekezwa na kamati ya upatanishi, Spika wa Bunge la Kitaifa atautuma Mswada huo kwa Rais katika siku saba ili uidhinishwe.
(4)Ikiwa kamati ya upatanishi itakosa kuafikiana kuhusu toleo hilo la Mswada katika kipindi cha muda wa siku thelathini, au iwapo toleo hilo lililopendekezwa na kamati litakataliwa na mojawapo ya Vitengo vya Bunge, basi Mswada huo utakuwa umeshindwa.