Haki za raia
(1)Kila raia anastahiki––
(a)kupata haki, fadhila na manufaa ya uraia kulingana na udhibiti uliowekwa au kama inavyoruhusiwa na Katiba hii; na
(b)kupata pasipoti ya Kenya na hati yoyote ya usajili au utambulisho unaotolewa na Taifa kwa raia.
(2)Pasipoti au hati nyingine inayorejelewa katika ibara ya (1) (b) inaweza kutopeanwa kwa mtu, matumizi yake kusimamishwa au kupokonywa tu kulingana na Sheria ya Bunge ambayo inatosheleza vigezo vilivyotajwa katika Kifungu cha 24.