Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 122

Kif.122

Kupiga Kura Bungeni

(1)Suala lolote litakalopendekezwa ili kuamuliwa katika mojawapo ya Vitengo vya Bunge, litaamuliwa na walio wengi katika Kitengo hicho, ambao wamehudhuria na kupiga kura, isipokuwa Katiba inapoagiza vinginevyo.

(2)Katika swali linalopendekezwa ili kuamuliwa katika mojawapo ya Vitengo vya Bunge—

(a)Spika hatapiga kura; na

(b)iwapo kura zitakuwa sawa katika pande zote, swali hilo litakuwa limeshindwa.

(3)Mwanachama hatapigia kura suala lolote ambalo ana maslahi ya kifedha kwalo.

(4)Katika kubaini idadi ya wanachama katika Kitengo cha Bunge kwa madhumuni yoyote ya upigaji kura katika Kitengo hicho, Spika wa Kitengo hicho hatahesabiwa kama mwanachama.

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho