Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 126

Kif.126

Eneo la vikao vya Bunge

(1)Vikao vya Kitengo chochote cha Bunge vinaweza kufanyiwa sehemu yoyote nchini Kenya, na kuanza kwa wakati wowote utakaoteuliwa na Bunge.

(2)Kila kutakapochaguliwa Bunge jipya, Rais, kwa kutoa notisi katika Gazeti Rasmi la Serikali, atateua mahali na tarehe ya kikao cha kwanza cha Bunge jipya, ambayo haitakuwa zaidi ya siku thelathini baada ya uchaguzi mkuu.

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho