Uraia kwa kuzaliwa
(1)Mtu ni raia kwa kuzaliwa ikiwa katika siku yake ya kuzaliwa, bila kujalisha ikiwa mtu huyo amezaliwa nchini Kenya, baba au mama wa mtu huyo ni raia.
(2)Ibara ya (1) pia inatumika kwa mtu ambaye amezaliwa kabla ya tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba hii, bila kujalisha iwapo mtu huyo alizaliwa nchini Kenya, ikiwa mama au baba ya mtu huyo ni raia, au alikuwa raia.
(3)Bunge linaweza kutunga sheria ili kudhibiti athari za sehemu ya (1) na (2) kwa vizazi vya raia wa Kenya ambao wamezaliwa nje ya Kenya.
(4)Mtoto anayepatikana nchini Kenya ambaye anaonekana kuwa mwenye umri wa chini ya miaka nane, na ambaye uraia wake na wazazi wake hawajulikani, atachukuliwa kuwa raia wa Kenya kwa kuzaliwa.
(5)Mtu ambaye ni raia wa Kenya kwa kuzaliwa na ambaye katika tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba hii, amekoma kuwa raia wa Kenya kwa sababu mtu huyo alipata uraia wa nchi nyingine ana haki ya kurejeshewa uraia wa Kenya, kwakutuma ombi.