Uraia kwa kujiandikisha
(1)Mtu ambaye ameolewa na raia wa Kenya au ameoa raia wa Kenya kwa muda wa angalau miaka saba ana haki ya kusajiliwa kama raia kwa kutuma ombi.
(2)Mtu ambaye amekuwa mkazi nchini Kenya kihalali kwa muda wa miaka saba mfululizo, na ambaye anatimiza masharti yote yaliyotolewa na Sheria ya Bunge, anaweza kutuma ombi ili kusajiliwa kama raia.
(3)Mtoto ambaye si raia wa Kenya, lakini anapewa malezi na raia, ana haki ya kusajiliwa kama raia atumapo ombi.
(4)Bunge litatunga sheria itakayotoa masharti ambayo yatazingatiwa ili kuwapa uraia watu binafsi ambao ni raia wa nchi zingine.
(5)Kifungu hiki kinatumika kwa mtu kuanzia tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba hii, lakini mahitaji yoyote ambayo ni lazima yatimizwe kabla ya mtu huyo kustahiki ili kusajiliwa kama raia, yatachukuliwa kuwa yametimizwa pasi na kuzingatia ikiwa mtu huyu aliyatimiza kabla au baada ya tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba hii, au kwa kiwango fulani kabla, na kwa kiwango fulani baada ya tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba hii.