Mamlaka ya mahakama
(1)Mamlaka ya Mahakama yametolewa na wananchi na yatatekelezwa na mahakama na taasisi zilizo na mamlaka ya mahakama zilizobuniwa chini ya Katiba hii.
(2)Katika kutekeleza mamlaka ya mahakama, mahakama na taasisi zilizo na mamlaka ya mahakama zitaongozwa na kanuni zifuatazo—
(a)haki itatendewa wote, bila kuzingatia hadhi;
(b)utekelezaji wa haki hautacheleweshwa;
(c)njia mbadala za kusuluhisha kesi, ikijumuisha upatanishi, mashauriano, maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha mizozo zitakuzwa, lakini kulingana na ibara ya (3);
(d)haki itatekelezwa bila kuzingatia kwa uzito changamoto za kiutaratibu; na
(e)lengo na kanuni za Katiba hii zitalindwa na kukuzwa.
(3)Mbinu za kitamaduni za kusuluhisha mizozo hazitatumiwa kwa njia ambayo—
(a)inakiuka Sheria za Haki;
(b)Haikubaliki kimaadili na katika haki au inayosababisha matokeo ambayo sio ya haki au yasiyokubalika kimaadili;
(c)haiambatani na Katiba hii au na sheria yoyote iliyoandikwa.