Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi · Kitengo cha Serikali Kinachosimamia Mahakama

Kifungu cha 162

Kif.162

Mfumo wa mahakama

(1)Mahakama za ngazi ya juu ni Mahakama ya Juu Zaidi, Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu na mahakama zilizotajwa katika ibara ya (2).

(2)Bunge litabuni mahakama zenye hadhi ya Mahakama Kuu ili kusikiliza na kuamua mizozo inayohusu—

(a)ajira na mahusiano ya kikazi; na

(b)mazingira, matumizi, hatimiliki na umiliki wa ardhi.

(3)Bunge litaamua mamlaka na majukumu ya mahakama zinazobainishwa katika ibara ya (2).

(4)Mahakama za ngazi ya chini ndizo mahakama zilizobuniwa chini ya Kifungu cha 169, au zilizobuniwa na Bunge kulingana na Kifungu hicho.

Isome ndani ya Sura ya Kumi →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho