Mahakama ya Rufaa
(1)Mahakama ya Rufaa imebuniwa, ambayo—
(a)itakuwa na idadi ya majaji ambao hawatapungua kumi na wawili kulingana na Sheria ya Bunge; na
(b)itapangwa na kusimamiwa kulingana na mwongozo utakaotolewa na Sheria ya Bunge.
(2)Kutakuwa na Rais wa Mahakama ya Rufaa ambaye atachaguliwa na majaji wa Mahakama ya Rufaa kutoka miongoni mwao.
(3)Mahakama ya Rufaa ina mamlaka ya kusikiliza kesi za rufaa kutoka—
(a)Mahakama Kuu; na
(b)Mahakama au taasisi yoyote nyingine iliyo na mamlaka ya mahakama kama itakavyoagizwa kupitia kwa Sheria ya Bunge.