Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi · Kitengo cha Serikali Kinachosimamia Mahakama

Kifungu cha 167

Kif.167

Kipindi cha kuhudumu ofisini cha Jaji Mkuu na majaji wengine

(1)Jaji atastaafu kutoka ofisini atakapofikisha umri wa miaka sabini, lakini anaweza kuamua kustaafu wakati wowote baada ya kufikisha miaka sitini na mitano.

(2)Jaji Mkuu atahudumu ofisini kwa jumla ya miaka kumi au hadi atakapostaafu chini ya ibara ya (1), kustaafu huko kukizingatia itakayotimia mwanzo.

(3)Ikiwa muhula wa Jaji Mkuu wa kuhudumu utakamilika kabla ya Jaji Mkuu kufikisha umri wa kustaafu chini ya ibara ya (1), Jaji Mkuu anaweza kuendelea kuhudumu kama jaji wa Mahakama ya Juu Zaidi.

(4)Ikiwa, wakati wa kukamilika kwa muhula wa kuhudumu kwa Jaji Mkuu, Jaji huyo ataamua kuendelea kuhudumu mahakamani chini ya ibara ya (3), mtu atakayeteuliwa kama Jaji Mkuu atateuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 166 (1) ingawa uteuzi huo unaweza kusababisha idadi ya majaji kuzidi idadi inayokubalika ya majaji wa Mahakama ya Juu Zaidi.

(5)Jaji Mkuu na jaji mwingine yeyote anaweza kujiuzulu kutoka ofisini kwa kumwandikia Rais notisi.

Isome ndani ya Sura ya Kumi →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho