Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi · Kitengo cha Serikali Kinachosimamia Mahakama

Kifungu cha 169

Kif.169

Mahakama ndogo

(1)Mahakama za ngazi ya chini ni—

(a)mahakama za Mahakimu;

(b)mahakama za Kadhi;

(c)Mahakama za Kijeshi; na

(d)mahakama yoyote nyingine au taasisi itakayobuniwa kwa Sheria ya Bunge, isipokuwa mahakama zilizobuniwa inavyohitajika chini ya Kifungu cha 162 (2). (2) Bunge litatunga sheria itakayotoa mamlaka, na majukumu ya mahakama ambazo zimebuniwa chini ya ibara ya (1).

Isome ndani ya Sura ya Kumi →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho