Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi · Kitengo cha Serikali Kinachosimamia Mahakama

Kifungu cha 172

Kif.172

Kazi ya Tume ya Huduma za Mahakama

(1)Tume ya Huduma za Mahakama itahakikisha na kuimarisha uhuru na uwajibikaji wa kitengo cha mahakama, na kuimarisha utekelezaji bora wa haki, ulio wazi na wenye ufanisi na—

(a)itapendekezea Rais watu watakaoteuliwa kama majaji;

(b)itakagua na kutoa mapendekezo kuhusu masharti ya kuhudumu kwa—

(i)majaji na maafisa wengine wa mahakama, kando na mishahara yao; na

(ii)wafanyakazi katika kitengo cha mahakama;

(c)itateua, kupokea malalamishi, kuchunguza na kuwaondoa ofisini au vinginevyo kuwachukulia hatua za kinidhamu wasajili, mahakimu, maafisa wengine wa mahakama na wafanyakazi wengine katika kitengo cha mahakama, kwa namna ambayo imebainiwa na Sheria ya Bunge;

(d)itandaa na kutekeleza programu za elimu na mafunzo yanayoendelea kwa majaji, mahakimu na maafisa wengine mahakama; na

(e)itaishauri serikali ya kitaifa kuhusu uboreshaji wa utendakazi katika utekelezaji wa haki.

(2)Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume itaongozwa na yafuatayo—

(a)ushindani na michakato yenye uwazi katika uteuzi wa maafisa wa mahakama na wafanyakazi wengine katika kitengo hicho cha mahakama; na

(b)ukuzaji wa usawa wa kijinsia.

Isome ndani ya Sura ya Kumi →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho