Haki na uhuru wa kimsingi
(1)Sheria za Haki ni kiungo muhimu katika utawala wa kidemokrasia nchini Kenya na ndio msingi wa sera za kijamii kiuchumi na kitamaduni.
(2)Lengo la kutambua na kulinda haki za binadamu na uhuru wa kimsingi ni ili kulinda hadhi ya watu binafsi na jamii tofauti na kukuza haki za kijamii na kufanikisha uwezo wa binadamu wote.
(3)Haki na uhuru wa kimsingi katika Sheria za Haki—
(a)ni za kila mtu na wala hazitolewi na Serikali;
(b)hazitengi haki zingine na uhuru wa kimsingi ambazo haziko katika Sheria za Haki, lakini zinazotambuliwa au kutolewa na sheria, isipokuwa kwa kiwango ambacho haki hizo na uhuru haziambatani na Sura hii; na
(c)zinadhibitiwa tu kulingana na udhibiti uliobainiwa katika Katiba hii.