Mamlaka ya mahakama katika kudumisha na kutekeleza Sheria za Haki
(1)Kwa mujibu wa Kifungu cha 165, Mahakama Kuu ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi zinazoomba haki dhidi ya kunyimwa, kukiukwa, kuvunjwa au kutishiwa kwa haki au uhuru wa kimsingi katika Sheria za Haki.
(2)Bunge litatunga sheria ili kutoa uwezo wa kiasili kwa mahakama za ngazi ya chini katika usikilizaji na kuamuliwa kwa kesi zinazoomba haki dhidi ya kunyimwa, kuvunjwa, kukiukwa au kutishiwa kwa haki au uhuru wa kimsingi katika Sheria za Haki.
(3)Katika kesi yoyote iliyowasilishwa chini ya Kifungu cha 22, mahakama inaweza kutoa uamuzi unaofaa, ikijumuisha––
(a)kutangaza haki;
(b)kutoa amri ya kusitisha kitendo kinachokiuka haki za mtu aliyewasilisha kesi;
(c)kutoa amri ya kudumisha hali jinsi ilivyo;
(d)kutoa tangazo au tamko kuhusu ubatili wa sheria yoyote ambayo inanyima, inakiuka au kutishia haki au uhuru wa kimsingi katika Sheria za Haki na ambayo haijathibitishwa kulingana na Kifungu cha 24;
(e)amri ya fidia; na
(f)amri ya mahakama ya kukagua hatua za kitawala zilizochukuliwa na shirika la umma.