Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi na Tatu · Huduma kwa Umma

Kifungu cha 233

Kif.233

Tume ya Huduma za Umma

(1)Tume ya Huduma za Bunge Imebuniwa.

(2)Tume ya Huduma za Umma inajumuisha mwenyekiti, naibu mwenyekiti na wanachama wengine saba walioteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa.

(3)Kwa kuzingatia ibara ya (4), mtu hastahiki kuteuliwa kama mwanachama wa Tume hiyo ikiwa mtu huyo––

(a)ndani ya miaka mitano iliyopita, amehudumu au kugombea uchaguzi kama—

(i)mbunge katika Bunge la Kitaifa au mwakilishi wadi katika bunge la kaunti; au

(ii)mwanachama katika idara ya uongozi wa chama cha kisiasa; au

(b)anahudumu katika ofisi yoyote ya Serikali;

(c)anagombea, au kwa wakati wowote mwingine amewahi kugombea kuwa mwanachama katika Bunge la Kitaifa au katika bunge la kaunti; au

(d)anahudumu, au kwa wakati wowote mwingine , amewahi kuhudumu katika shirika la kisiasa linalofadhili au kuunga mkono mgombeaji wa uanachama katika Bunge la Kitaifa au bunge la kaunti.

(4)Ibara ya (3) (c) na (d) hazitatumika iwapo uchaguzi mkuu umefanywa mara mbili tangu mtu huyo alipogombea kiti au alipohudumu ofisini.

(5)Kutakuwepo na katibu wa Tume hiyo.

(6)Katibu––

(a)ndiye mtendaji mkuu katika Tume; na

(b)atateuliwa na Tume kwa muhula wa miaka mitano na anaweza kuteuliwa tena mara moja tu.

Isome ndani ya Sura ya Kumi na Tatu →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho