Ulinzi wa wafanyakazi wa umma
Afisa wa umma—
(a)hataonewa au kubaguliwa kwa kutekeleza majukumu ya kiofisi kulingana na Katiba hii au sheria nyingine yoyote; au
(b)hatafutwa kazi, kuondolewa ofisini au kushushwa cheo au kuchukuliwa hatua za kinidhamu bila mchakato uliopo wa kisheria kufuatwa.