Taasisi za usalama wa kitaifa
(1)Vitengo vya usalama wa kitaifa ni—
(a)Vikosi vya Ulinzi wa Kenya;
(b)Huduma za Upelelezi za Kitaifa; na
(c)Huduma za Polisi za Kitaifa.
(2)Lengo la kimsingi la vitengo vya usalama wa kitaifa na mfumo wa usalama ni kukuza na kutoa hakikisho kuhusu usalama wa kitaifa kulingana na kanuni zilizotajwa katika Kifungu cha 238 (2).
(3)Katika kutekeleza majukumu na mamlaka yao, vitengo vya usalama wa kitaifa na kila mwanachama wa vitengo hivyo vya usalama wa kitaifa—
(a)hatahudumu kwa njia inayopendelea;
(b)hataendeleza maslahi au malengo ya chama chochote cha kisiasa; au
(c)kuhujumu maslahi ya kisiasa au malengo ya kisiasa ambayo ni halali chini ya Katiba hii.
(4)Hakuna mtu atakayebuni kikosi cha kijeshi au kikosi chenye hadhi ya kijeshi au shirika linalodai kuendeleza na kutoa hakikisho kuhusu usalama wa kitaifa isipokuwa inavyoruhusiwa na Katiba hii au Sheria ya Bunge.
(5)Vitengo vya usalama wa kitaifa vitakuwa chini ya mamlaka ya kiraia.
(6)Bunge litatunga sheria itakayotoa mwongozo kuhusu majukumu, utaratibu na usimamizi wa vitengo vya usalama wa kitaifa.